
Ancelotti amwagia sifa Mbappe
Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema kuwa mshambuliaji nyota Kylian Mbappe anaweza kuwa gwiji katika klabu hiyo kama mfungaji bora wa muda wote Cristiano Ronaldo.
Mbappe ni mchezaji anayemkubali Ronaldo alipokuwa akikua na baada ya kujiunga na Madrid kutoka Paris Saint-Germain majira ya joto yaliyopita, amefikia jumla ya mabao 33 ya mshambuliaji huyo wa Ureno katika msimu wake wa kwanza Santiago Bernabeu.
"Ninachotamani kwa Mbappe ni kwamba ana uwezo wa kufikia kile Ronaldo alifanya akiwa Real Madrid na nadhani anaweza kufanya hivyo," Ancelotti aliambia mkutano wa wanahabari.
"Hiyo inamaanisha kuwa atakuwa gwiji wa Real Madrid, kama Cristiano Ronaldo." Ronaldo alijiunga na Real akitokea Manchester United mwaka 2009 na akaondoka mwaka 2018 akiwa mfungaji bora wa klabu hiyo akiwa amefunga mabao 450.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40, ambaye sasa yuko Al-Nassr nchini Saudi Arabia, alifunga mabao 33 katika michezo 35 katika kampeni yake ya kwanza akiwa na Real Madrid.
Mbappe, mwenye umri wa miaka 26, alifunga mabao mawili dhidi ya Leganes kwenye LaLiga Jumamosi na akasema ilikuwa "ya kipekee sana" kulinganisha na Ronaldo.
Huku Madrid wakiwa bado wanachuana katika nyanja tatu msimu huu Mbappe ana muda mwingi wa kuongeza idadi yake.
Kikosi cha Ancelotti kinaikaribisha Real Sociedad Jumanne kwenye mechi ya mkondo wa pili ya nusu fainali ya Copa del Rey, wakiwa mbele kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa San Sebastian.
Iwapo Madrid wangeshinda kombe hilo, Ancelotti atakuwa kocha wao wa kwanza kulinyanyua mara tatu.
“Kukaribia fainali kunanipa motisha, kunawapa wachezaji motisha na kunaipa klabu motisha,” alisema Ancelotti.
"Ni mafanikio kucheza fainali katika shindano lolote, kwa hivyo kuwa karibu sana, kuwa na faida ndogo, na kwa sababu tutapata uungwaji mkono na mashabiki wetu bila shaka hututia motisha zaidi."